Na tukawahukumia Wana wa Israili katika Kitabu kwamba: Hakika nyinyi mtafanya fisadi katika nchi mara mbili, na kwa yakini mtapanda kiburi, kiburi kikubwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na tuliwapasha habari Wana wa Isrāīl katika Taurati ambayo waliteremshiwa kwamba yeye hapana budi itatukia kutoka kwao uharibifu mara mbili katika Bayt al- Maqdis na sehemu zinazofuatia kwa kudhulumu, kuua Manabii, kufanya kiburi, kupita kiasi na kufanya uadui.